TRENDING NOW

06:14 AM Audio | Rayvanny - Natafuta


Maswali ya Jaji Rumanyika kwa Lulu Kuhusu Kesi Inayomkabili ya Kuua Bila Kukusudia
BAADA YA Muigizaji, Elizabeth Michael ‘Lulu’kuanza kujitetea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Steven Kanumba bila kukusudia, msanii huyo amekana kuhusika na kifo hicho.
Lulu ameeleza siku ya tukio, Kanumba alikuwa amelewa na yeye Lulu alitaka kutoka na marafiki zake lakini alimkataza, baada ya Kanumba kuona simu ya Lulu imeita alizani anaongea na mwanamme mwingine huku ambapo alichukua panga na kumkimbiza nalo. Kanumba alianguka na Lulu kuchukua gari na kukimbilia Coco Beach ambapo baadaye alikamatwa na polisi maeneo ya Bamaga.
Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika amemtwanga maswali Lulu kama ifuatavyo;
Jaji Sam Rumanyika: Kipindi unaendesha gari ulikuwa na leseni halali?
Lulu: Ndiyo.
Jaji: Tufafanulie uhalali wake.
Lulu: Nilikuwa sina.
Lulu: Baada ya kukamatwa nilipelekwa kituo cha polisi Oysterbay nilikuwa nikihojiwa nikiwa sijui kama Kanumba amefariki.

>>>>PIA SOMA HII>>>>Daktari: Tulifungua Ubongo wa Kanumba na Kuukuta Umevimba na Kisogo Kilikuwa na Mgando wa Damu

No comments:

Post a Comment