TRENDING NOW

06:14 AM Audio | Rayvanny - Natafuta


Lowassa Amemtembelea Tundu Lissu Kumjulia Hali
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa amemtembelea kumjulia hali Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Mhe. Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibu Nairobi nchini Kenya. 

Mhe. Lowassa ameongozana mke wake Mama Regina Lowassa ambapo leo hii walifika hospitalini hapo kumjulia hali Mhe. Lissu 

Tangu picha za Lissu kuanza kuonakana pindi watu wanapoenda kumjulia hali, viongozi wa juu na wabunge wamekuwa wakifanya hivyo. Miongoni mwao ni mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, Mhe. John Heche na mbuge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ambao hivi karibuni wameonekana wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment